Unknown Unknown Author
Title: Boko Haram wapigana wenyewe kwa wenyewe Nigeria
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamepigana wenyewe kwa wenyewe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, duru za kiu...
Abubakar Shekau
Wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamepigana wenyewe kwa wenyewe kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, duru za kiusalama zimeambia BBC.
Maelezo kuhusu mapigano hayo yaliyotokea katika eneo la Monguno, jimbo la Borno karibu na Ziwa Chad bado ni finyu kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano ya simu za mkononi maeneo hayo.
Mapigano yametokea baada ya kundi linalojiita Islamic State (IS) kutangaza mwezi uliopita kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram, na kumuondoa Abubakar Shekau.
Lakini Bw Shekau, ambaye awali alikuwa ametangaza kujiunga na IS, alisema bado anaongoza kundi hilo.
Baadhi ya wachanganuzi wanasema mgawanyiko katika kundi hilo huenda ukawafaa wanajeshi wa Nigeria katika juhudi zao za kukabiliana na wanamgambo hao.
Kufikia sasa, jeshi la Nigeria halijatamka lolote kuhusiana na mapigano hayo.
Source bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top