Unknown Unknown Author
Title: Kurugenzi mawasiliano ikulu yabaini barua feki
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imewatahadharisha watanzania kuwa kuna watu wanatumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Iku...
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imewatahadharisha watanzania kuwa kuna watu wanatumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi hiyo imesema watu wamekuwa wakiwataka wahusika wanaopelekewa barua hizo kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016".
Taarifa imesema kuwa barua hizo zilizotiwa saini na mhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.
Aidha taarifa hiyo imewataka watu waliopokea barua hizo wazipuuze na wachukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.
Source eatv

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top