Unknown Unknown Author
Title: MADHARA YA KUTAZAMA PICHA NA VIDEO ZA UCHI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha za uchi  pamoja na  video za uchi  ( Ponografia au ngono ), Kwa kizazi hiki zimeenea kila kona katika  televisheni, sinema, Simu, Com...

Picha za uchi pamoja na video za uchi (Ponografia au ngono), Kwa kizazi hiki zimeenea kila kona katika televisheni, sinema, Simu, Computer, video za miziki na internet pia. Je! Picha na video izo za ngono hazina madhara kwetu, kama wengi tunavyo dhani?

Leo tutatazama madhara ya picha/Video za uchi (Ngono) kwa vijana, katika makala nyingine tutatazama adhari za picha izo kwa watu wazima, kisha adhari za picha za uchi katika mahusiano.


Madhara ya kutazama picha/video za uchi (Ponografia) kwa Vijana. Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa picha/Video za uchi (ponografia) ni vijana chipukizi, hasa wavulana wenye umri wa miaka kati ya 12-17. Asilimia kubwa ya vijana hao hujifunza na kujiingiza katika  maswala ya ngono, wakiwa katika umri mdogo huku chanzo kikiwa na picha/video hizo za uchi. 
Baada ya vijana hao kujifunza na kuingia katika maswala ya ngono kitu kinachofuata ni ongezeko la mimba zisizo rasmi kwa hawa vijana wadogo "Matineja" na kuongeza kasi ya magonjwa yanayoambukizwa kupitia zinaa kama vile UKIMWI n.k. huku chazo kikiwa ni picha/video hizo uchi ambao watoto wetu wanazo kwenye simu na laptop zao.

“Uchunguzi wa athari za sauti na picha za uchi (Ponografia) katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama picha hizo huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.” Alisema Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top