Unknown Unknown Author
Title: Maganda ya chungwa'' yamshindia tuzo la Google
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msichana wa miaka 16 nchini Afrika Kusini amejishindia zawadi ya maonyesho ya Google kwa kutumia maganda ya chungwa kutengeza kifaa kinach...
Kiara Nirghin
Msichana wa miaka 16 nchini Afrika Kusini amejishindia zawadi ya maonyesho ya Google kwa kutumia maganda ya chungwa kutengeza kifaa kinachosaidia udongo kuhifadhi maji.
Kiara Nirghin aliwashinda wanafunzi wengine duniani kwa kujipatia ufadhili wa masomo wenye thamani ya dola 50,000 kwa ''kukabiliana na kiangazi kupitia chungwa''.
Kazi yake inajiri kufuatia kiangazi ambacho kinaendelea kuathiri Afrika Kusini.
Maganda ya chungwa yamshindia tuzo la Google
Image captionMaganda ya chungwa yamshindia tuzo la Google
Kiangazi hicho ambacho ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu 1982 kimeathiri mimea huku mifugo ikifariki.
Kwa sasa anatumai kwamba mbinu hiyo inaweza kuwasaidia wakulima kuhifadhi fedha pamoja na mimea.
bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top