Ligi ya klabu bingwa barani ulaya imeendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na michezo tisa ikipigwa katika viwanja tofauti.
Manchester City wakiwa nyumbani wameibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, hatrick ya Kun Aguero na goli moja la Kelechi Iheanacho yalitosha kuipatia Man City alama tatu na kuwa timu ya pili kwenye msimamo wa kundi C ambalo linaongozwa na Barcelona.
Tottenham Hotspurs ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa ambayo inaongoza ligi kuu nchini humo.
Lakini usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni kicheko kwa wachezaji na washabiki wa Leicester City, wakiwa ugenini waliipiga Club Brugge ya ubelgiji jumla ya magoli 3-0 huku Riyad Mahrez akifunga mara mbili.
Borussia Dortmund ikiwa ugenini iliidhalilisha Legia Warszawa ya Poland kwa dozi ya 6-0.
Na katika mchezo uliowastaajabisha wengi ulikuwa ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP Lisbon ya ureno ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Sporting Lisbon ilikuwa ya kwanza kuandika goli kwenye dakika ya 48 goli lililodumu hadi dk ya 89 ya mchezo ambapo C.Ronaldo aliisawazishia timu kwa mpira wa adhabu ndogo maridadi kabisa uliyoenda moja kwa moja kimiani, sekunde chache kabla mpira kumalizika Alvaro Morata aliiandikia Real Madrid goli la pili akiunganisha krosi ya James Rodriguez.
Matokeo mengine
Bayern 04 Leverkusen 2-2 CSKA Moscow
FC Porto 1-1 F.C. Copenhagen
Juventus 0- 0 Sevilla
Lyon 3-0 Dinamo Zagreb
Source bbc
Post a Comment