Unknown Unknown Author
Title: Nay Wa Mitego afunguka kuhusu Ndoa ya Shamsa Ford
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameitabiria mema ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford. Shamsa ambaye alikuwa m...
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego ameitabiria mema ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford.
nay wa mitego922
Shamsa ambaye alikuwa mpenzi wa rapper huyo alifunga ndoa mwezi mmoja uliopita na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay Wa Mitego amesema Shamsa ni ‘wife material’ hivyo anamtabiria kudumu katika ndoa yake.
“Ndoa ni kitu cha heri lakini sometime watu wanaweza wakaoana kwa kutafuta experience za ndoa zinakuwaje, watu wakioana inakuwaje, ukishapata experience kila mtu anaendelea kupuyanga,” alisema Nay. “Sasa mimi sijajua kama wao wanatafuta experience za ndoa ili kujua watu wakioana wanakuwaje,”
Aliongez, “Kwa jinsi ninavyomjua Shamsa ni mwanamke kweli, kwa sababu ni mwanamke ambaye anastahili kuwa mke kwa sababu amekaa ‘kiwife material’ kiukweli kabisa, sijui mtu ambaye ameenda kuolewa naye na kuna vitu yeye mwenyewe anatakiwa kubadilika,”
Rapper huyo amedai Shamsa kabla hajaolewa alimwambia kwamba anaenda kuolewa na akampatia baraka zote.
SHAMSA FORD22

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top