ZIJUE SABABU ZA MASTAA WENGI KUTODUMU KATIKA MAHUSIANO.
Mastaa wengi wamekuwa hawadumu kwenye ndoa zao na wengine kwenye uhusiano wao wa kimapenzi. Ukijaribu kumuuliza kijana yeyote mwenye nia ya kuoa atakuambia bora aoe mwanamke wa kawaida kuliko staa.
Tamaa
Hili lipo sana kwa mastaa wa kike. Baadhi yao wana tamaa ya kuwa na maisha fulani ili waonekane nao wamo wakati uwezo haupo. Matokeo yake sasa akiolewa na mwanaume ambaye hana kitu, akimpata wa pembeni ‘pedeshee’ wa kumtunza, kwa tamaa zao hujikuta wakisaliti.
Unakuta msichana kwa kuwa ni staa, anataka awe na gari zuri, abadili nguo kila siku, simu kali na vitu vingine vya thamani wakati pesa hana na mume naye ni kapuku. Hapo ndipo wengi huamua kuchepuka na matokeo yake sasa hajali tena ndoa.
Ustaa mwingi
Mastaa wengi wakishajitambua kuwa wao maarufu, basi hata kwa wapenzi wao wanaleta zile nyodo za ustaa. Wanasahau kuwa hata rais anapokuwa na mkewe humnyenyekea kama mke na mambo mengine kuendelea.
Utakuta staa anataka kuonesha ustaa wake kwa mumewe, yaani anataka mume awe chini yeye awe juu kisa tu anatikisa jiji.
Starehe kwa sana.
Mke wa mtu hata kama anastahili kustarehe siku mojamoja, lakini baadhi ya mastaa walioingia kwenye ndoa huona wao starehe lazima ichukue sehemu kubwa ya maisha yao. Atalazimisha kila siku watoke na hata kama mume atakuwa si mtu wa kuendekeza mambo hayo, yeye ataomba awe anaenda na mastaa wenzake, akikataliwa inakuwa tatizo.
Hawajitambui.
Mastaa wengi wanakosa elimu ya kujitambua. Ndiyo maana wengi wanaitwa malimbukeni. Unakuta staa amepata mume mzuri tu lakini yeye anashindwa kujitambua kuwa yeye ni mke wa mtu asiyestahili kuingiza ustaa wake kwenye maisha yake ya nyumbani.
Ndoa fasheni.
Jaribu kuchunguza utagundua kuwa, mastaa wengi wanaolewa kama fasheni. Utamkuta staa wa kike anasema wazi kwamba, amechangia wengi sana hivyo na yeye anataka kuchangiwa hivyo analazimisha kuolewa.
Wanaoolewa kwa sababu hiyo ni wale ambao hata ndoa zao zikivunjika hawaoni hatari, wanaona ni sawa tu kwa sababu angalau wameonja ndoa!
Wanakosa staha.
Mke kama mke lazima awe na staha, kitu ambacho baadhi ya mastaa wanakikosa. Utakuta staa kaolewa lakini ana marafiki wengi wa kiume na anataka mume wake asihoji juu ya urafiki wao.Kama ni msanii akiwa lokesheni, afanyiwe lolote na wanaume, avae nguo hata za utupu kisa eti anaigiza. Mbaya zaidi si lokesheni, hata nje ya fani wanataka kuishi kisanii
Wako tayari kuachika.
Mastaa wengi wa kike wakiolewa, wanakaa mkao wa kuachika wakati wowote. Ni wachache wanaofanya jitihada za kutunza ndoa zao. Yaani wanatembea kwenye ile dhana potofu kwamba staa hawezi kudumu kwenye ndoa.
Post a Comment