Unknown Unknown Author
Title: ALICHOSEMA MBOWE KUHUSU VIONGOZI WAO WA CHADEMA WALIOHUKUMIWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leo hii tumepata taarifa za kusikitisha sana, kwamba Mwenyekiti wetu wa Chama wa Mkoa wa Lindi pamoja na Katibu wa kijiji kimojawapo kul...



Leo hii tumepata taarifa za kusikitisha sana, kwamba Mwenyekiti wetu wa Chama wa Mkoa wa Lindi pamoja na Katibu wa kijiji kimojawapo kule Lindi, Ndugu Suleiman Mathew amehukumiwa kwenda jela bila faini kwa miezi nane (8) Mtakumbuka ni wiki iliyopita tu Mbunge wetu wa Kilombero nae amehukumiwa kwenda jela miezi sita (6) bila faini, wanahukumiwa kwenda jela bila faini kwenye makosa ambayo kimsingi yana adhabu za faini kwa nia ya kuwakomoa.
Vifungu vya mashtaka walivyoshtakiwa navyo vinaruhusu hukumu ama faini, lakini inaonekana sasa wanahukumiwa bila faini kwa nia ya kuwakomoa, sasa viongozi wetu ambao tunajua ni potential kama Suleiman Mathew,anashtakiwa eti kwa kosa la kufanya mkutano wakati yeye ni Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa,Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa unapofanya mkutano na wanachama wako unaweza ukakamatwa ukafungwa eti unafanya mkutano bila kibali ni jambo la kusikitisha wakati tunajua ndani ya serikali ya Chama cha Mapinduzi viongozi wake wengi wanafanya mikutano, sasa huu ni mkakati wa kudhoofisha upinzani na mkakati wa kuwatisha wapinzani waiogope siasa, waone siasa ya Upinzani kama vile ni kazi haramu.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top