Unknown Unknown Author
Title: Chocolate zinavyohusishwa na ‘uwezo wa akili’ kwa wanafunzi darasani
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa hi...

Wakati wazazi wengi nchini wakihaha kudhibiti ulaji holela wa vitu vitamu kwa watoto wao ili kuimarisha afya ya kinywa. utafiti mpya wa hivi karibuni umeibuia mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa watoto kufanya vizuri darasani.
Aidha, utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia kupunguza kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka kwa umri. Ripoti ya utafiti huo ilitolewa hivi karibuni, inabebwa na utambulisho usemao ‘ulaji wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo” na kwamba ”unaweza kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid kumtupa mkono’
Utafiti huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini kuwa kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu kuwa katika kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo hayo yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala aina nyingine za ulinganifu wa jumla wa kiafya .
Inaelezwa zidi kuwa utafiti huo unaonyesha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ulaji wa kila mara wa chocolate na matokeo ya majaribio kuhusu uwezo wa uubongo katika kufikiri hata hivyo utafiti huo haujathibitishwa kwa asilimia 100 juu ya uhakika wa kisayansi juu ya kile kilichobainishwa.
Aidhja imeonekana watu wanotumia zaidi chocolate walikuwa na lishe bora zaidi na pia kunywa pombe kwa kiasi kidogo, na makundi yote yalitegemea uwezo wa kukumbuka mambo kupitia kiwango chao cha ulaji wa Chocolate.
SOURCE: NIPASHE

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top