Unknown Unknown Author
Title: Je Diamond katimiza ahadi yake?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines siku ya February 1 2016 ni hii ya msanii wa Bongofleva na  CEO  wa record label ya Wasafi ...

Moja kati ya stori zilizoingia kwenye headlines siku ya February 1 2016 ni hii ya msanii wa Bongofleva na CEO wa record label ya Wasafi Classic Baby (WCB) Diamond Platnumzkuweka wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika atanunua gari aina ya Rolls Royce.
Kupitia account yake ya instagram usiku wa August 30 Diamond Platnumz alipost clip video ya Rolls Royce yenye kivuli cha sura yake, inawezekana Diamond akawa ametimiza ahadi yake ya kumiliki gari hilo kabla ya mwaka 2016 kumalizika, kamaDiamond atakuwa kanunua gari hilo atakuwa ni mtanzania wa pili anayefahamika kumilikiRolls Royce baada ya makamu mwenyekiti wa zamani wa Yanga Davies Mosha
Baadhi ya mastaa Afrika wanaomiliki gari aina ya Rolls Royce ni Koffi Olomide na staa wa soka wa zamani wa Arsenal Emmanuel Adebayor ambaye kwa sasa anaichezeaCrystal Palace, bado haijajulikana Rolls Royce aliyopost  Diamond ni toleo la mwaka gani ila stori kutoka autoguide.com inaeleza kuwa Rolls Royce inauzwa zaidi ya dola laki 3 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 600 pia inategemeana na toleo.
IMG_20160122_182043

Hili linamilikiwa na mtanzania Davies Mosha Roys Rolls PHANTOMS 2015

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top