Unknown Unknown Author
Title: KWA HILI MALINZI UMETUDANGANYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  MWEZI  Agosti 14 ya mwaka huu, Shirikisho La Mpira wa miguu mkoa wa Kagera lilifanya uchaguzi wa mkoa huo na kumpitisha Rais wa TF...

 


MWEZI Agosti 14 ya mwaka huu, Shirikisho La Mpira wa miguu mkoa wa Kagera lilifanya uchaguzi wa mkoa huo na kumpitisha Rais wa TFF, Jamal Emily Malinzi kuwa mwenyekiti wa KRFA kwa ushindi wa kura 21 kati ya kura 22 zilzopigwa.

Malinzi umefanya maamuzi magumu ambao kila mdau wa mpira anatamani kujua nini haswa kilichokusukuma ukaamua kugombea nafasi ya uwenyekiti ili hali ukiwa bado ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.

Umeamua kuvaa kofia mbili, moja kichwani na nyingine umeivalisha kwenye mgumi ya mkono wako wa kushoto, sehemu ambayo mimi nakukumbusha sio eneo stahiki zaidi ya lile la kichwani ambapo tayari ulishavaa kofia ile ya kwanza.

Nafahamu ni macho ndio yaliyokuvutia kununua kofia zote mbili ambazo sasa kwa tamaa ya kuvaa ili upendeze, inakushawishi uvae zote kwa wakati mmoja jambo ambalo pengine unaweza ukawa ni wa kwanza kulifanya tangu dunia hii iumbwe.

Labda nikukumbushe kama ulikuwa umesahau, kabla ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa KRFA, Malinzi ulikuwa na bado mpaka sasa ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu Nchini TFF, 

Ulizipitia kanuni na sheria za Baraza la Michezo la Taifa lakini hata zile za TFF? Bila shaka unazifahamum sema umeamua kufunga vioo vya gari ili ututimlie vumbi sie tusio na hatia.

Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za uongozi za BMT, Malinzi haukustahili hilo ulilolifanya Agosti 14. 

Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa Na. 12 ya  1967 na marekebisho yake ya Na. 6 ya 1971 pamoja na kanuni za BMT na kanuni za usajili za 1999, 8[1] zinasema,

“Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu mkuu, Katibu msaidizi na Mweka hazina wa chama cha mchezo wowote hatoruhusiwa kushika nafasi ya uongozi zaidi ya moja kwenye vyama tofauti vinavyoshughulikia aina moja ya mchezo” 

Lakini umebariki kura za wajumbe wa mkoa wa Kagera lakini pia ukiwa bado ni rais wa shilikisho la mpira wa miguu Tanzania, au kuna utofauti wa aina ya michezo kati ya TFF na KRFA? Hapo Malinzi umetuweka wengi kwenye mabano tusijue hata wapi tutatokea.

Aidha katika kifungu cha 8, kifungu kidogo cha 2 cha sheria hiyo kinasema, 

“Endapo viongozi waliotajwa katika kanuni ya 8 [1] watagombea na kupata uongozi kwenye ngazi nyingine ya chama cha mchezo huo huo, Watalazimika kuachia nafasi moja ya uongozi waliyokuwa wakishikilia na kubaki na moja tu”

Wakati mwingine, huu tunaiuita uchu wa madaraka kama bado hauna ndoto ya kuiuza kofia moja ili ubaki na ile moja uliyoivaa kichwani na ile ya kwenye ngumi ya mkono wa kushoto, waachie wengine watakaoona inawafaa.

Lakini umekaa kimya, kama vile hakuna kinachoendelea ndani ya mpira wa miguu nchini, na hata lile sakata la klabu ya Stand United umeona haina maana ila umeanzisha lako ambalo pengine ni la makusudi kwani kila kitu unakifahamu.

Mathalani, ukiwa kama mwenyekiti wa KRFA lakini pia ukiwa kama rais wa TFF, likiwa limetokea jambo la kusimama kama mwemyekiti wa mkoa kwa upande wa taifa ambako ndio unamkuta TFF, hapo limekaaje Malimzi?

Au, mfano mwingine wa kawaida sana, ile ishu ya Polisi Tabora na Mwadui FC. Kama moja ya timu hizi ingekuwa Kagera, kivuli cha mwenyekiti mkoa angesimama nani na kule upande wa TFF angekuwa nani? Hauoni hapo kunavyokuwa na mgongano wa maslahi?

Maamuzi yako yamepelekea watu kufikiri kila walichokifikiria na hata kuirudisha siasa ndani ya mpira wa miguu jamba ambalo nilikuwa nafikiri kuwa limeisha sasa  kumbe kiongozi mkubwa kama wewe unaamua kuirudisha tena.

Kuna haja gani ya kulilia mabadiliko kwenye michezo kama viongozi ndio wanaoongoza kwa kutengua sheria na kanuni zilizowekwa na baraza linalosimamia michezo nchini.

Hakiki umekuwa kinyume na matarajio ya wengi wanaotaka mabadilikoa na wewe mwenzetu ukiwa kama kiongozi hilo wala hujali kwani tayari hesabu zako za darasa la sita zilikwishatimia.

Yakupasa usimame kwa miguu yako mwenyewe na utamke kwa kinywa chako kama haya tunayosema tunakutwisha mzigo usio wako au ni sahihi tu hata ukikaa kimya.
source kunji tv

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top