Mahakama ya juu ya utawala nchini Ufaransa imeahirisha marufuku iliyowekwa na miji ya mwambao juu ya uvaaji wa vazi la kuogelea linalofunika mwili mzima ama burkini linalovaliwa na wanawake wa kiislamu.
Mahakama hiyo imeahirisha marufuku hiyo katika moja wapo ya miji hiyo wa - Villeneuve-Loubet - lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba karibu miji thelethi iliyoweka amri hiyo pamoja na maeneo mengine ya miji ya mwambao wakaondoa marufuku hiyo.
Kesi hiyo iliwasilishwa na wanaharakati ambao walisema hatua ya kupiga marufuku burkini inakiuka haki za wanawake wa kiislamu ya kuvaa kile wanachokitaka.
Mahakama itatoa uamuzi wa mwisho juu ya uhalali wa kisheria wa marufuku baadae.
Wakili mmoja nje ya mahakama aliwaambia watu waliotozwa faini kwa kuvaa vazi hilo wataweza kudai pesa zao zirejeshwe
Source bbc
Post a Comment