Suala la usawa wa kijinsia limekuwa likiongelewa katika maeneo tofauti na hata kuundwa kwa taasisi mbalimbali zitakazohakikisha kuwa kuna kuwepo na usawa huo. Lakini licha ya jitihada zote hizo bado kile kinachoelezwa kuwa ndio usawa wa kijinsia hakijafikiwa.
Mwanaume mmoja nchini Uganda aliamua kuishi kama mwanamke kwa wiki moja kuweza kujionea ni changamoto gani hasa wanawake wanakumbana nazo katika maisha ya kila siku. Tunapokuwa tunaona kuwa wanawake ndio hufanya kazi za nyumbani na kuwa mwanauume ndio kichwa cha familia na ndiye mwenye maamuzi y mwisho. Hii imeendelea kuwapo kwa sababu watoto wamekuwa wakiiga kile wakubwa wanachofanya bila hata ya wao kujua
Samuel Woira ambaye ni mtetezi wa haki za wanawake (Feminist) akielezea kilichotea na namna alivyoamua kuishi kama mwanamke ili kuzifahamu changamoto zao.
Nilipewa kazi za kufanya kila siku kutoka kwa wanawake waliokuwa wakinisimamia, baadhi zilikuwa ngumu lakini nyingine zilikuwa rahisi, marafiki zangu wakati mwingine walinicheka na baadhi kukataa kuzungumza na mimi, alisema Samuel. Aliendelea kusema kuwa siku ya kwanza alitakiwa kuhakikisha anafanya usafi ndani na kuosha vyombo kabla ya kwenda kazini, baada ya kumaliza hayo yote, kwa mara ya kwanza alichelewa kufika kazini.
Baada ya kufika kwa kuchelewa, baadhi ya rafiki zangu waliamini kweli wanawake huwa na kazi nyingi na hivyo wakaahidi kuwasaidia wake zao ili wawahi kazi lakini wengine walisema kama ninaigiza kuwa mwanamke nisifanye nao kazi. Nilitakiwa kuvaa wigi, nikachua la bluu, watoto mtaani walikuwa wakinicheka na kuniita ‘Aunt’ huku wakitaka nibadilishe sauti ninapozungumza nao, alielezea Samuel.
Siku nyingine nilitakiwa kukunja goti nikimsalimia mtu kama ishara ya heshima vile wafanyavyo wanawake wengi. Hii iliwafurahisha wanawake niliokutana nao na ilionyesha kuwa nao wanafurahi mtu anapoinama kidogo akiwasalimia. Wakati mwingine nilitakiwa kuweka machungwa kifuani kuwa kama maziwa. Nilipofanya hivyo sikuwa naweza kufanyakazi wala kutembea haraka, hata wasiamamizi wangu walichukizwa na uvivu wangu. Zaidi wanaume walikuwa wakiniita majina ya ajabu kama ‘Demu’, hii ilinionyesha ni kiasi gani wanawake hawapendi kuitwa majina hayo ya ajabu.
Niliendelea kufanya mambo mengi wayafanyayo wanawake, mfano kukaa chini wakati unakula, kufua, kufanya kazi za nyumbani unaporudi nyumbani ukiwa umechoka na nyingine nyingi, aliendelea kueleza Samuel.
Alihitimiesha kwa kusema kuwa, wiki hiyo moja aliyofanya kazi kama mwanamke alijionea kuwa wanawake wanafanya kazi hata zaidi ya wanaume, akasema ni wakati sasa wanaume kuwasaidia na kuamini kuwa wanawake wanaweza. Aidha aliwataka Wabunge, Madaktari, Wanasheria wa kike kuhakikisha wanapigania haki za wanawake wengine.
Wanawake wengi nilipowaeleza nilichokuwa nakifanya walifuahia na kusema huenda hilo lokawaamishisha wanaume kuwa wanawake pia wanaweza, alisema Samuel. Akitoa kauli yake ya mwisho aliema, kuzungumza tu hakutaleta usawa wa kijinsia, alisema sasa ni wakati wa Uganda kuungana kuhakikisha inafikia lengo la kuleta usawa wa kijinsia.
Chanzo Swahilitimes
Post a Comment