Unknown Unknown Author
Title: PAPA BENEDICT XVI AELEZA KWANINI ALIJIUZULU MWAKA 2013.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Papa Mtakatifu Benedict XVI alipokuwa akihojiwa alisema kuwa aliona kujiuzulu kwa ke lilikuwa ni jambo la lazima kutokana na kuporomoka kwa...
Papa Mtakatifu Benedict XVI alipokuwa akihojiwa alisema kuwa aliona kujiuzulu kwa ke lilikuwa ni jambo la lazima kutokana na kuporomoka kwa afya yake na kushindwa kuendana na kasi ya kazi zake.
Japo alitamani kumaliza muda wake wa utumishi, Papa alisema kuwa alipotembelea Mexico na Cuba Machi, 2012  alijiona kabisa hawezi tena kuendelea na safari hivyo ni vyema kuachia madaraka.
Alisema kuwa japo alifurahishwa na mapokezi katika nchi ya Mexico na Cuba, lakini huu ndio wakati alioona kuwa hawezi tena kuendelea kutekeleza majikumu yake hasa kusafiri safari za kimataifa. Hata alipotafuta ushauri wa Daktari wake, aliambiwa kuwa asingeweza kuhudhuria hafla ya Siku ya Vijana iliyofanyika Rio de Janeiro.
Papa alieleza kuwa, licha ya kua alikuwa akiifahamu hali yake, lakini mwaka 2005 alikubali alipochaguliwa akiamini kua alipaswa kumtumikia Mungu na kuwa yeye atamuwezesha kufanya kazi.
Papa Benedict XVI alichaguliwa  19 Aprili 2005 kisha akaapishwa kushika wadhifa huo 24 Aprili 2005 na kujiuzulu nafasi hiyo 28 Februari 2013.
Pope Benedict XVI greets the crowd after delivering his Christmas message "urbi et orbi" (to the city and the world) from the central balcony of St. Peter's Basilica at the Vatican Dec. 25. (CNS photo/Paul Haring) (Dec. 25, 2012) See POPE-CHRISTMAS to come.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top