Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Songea mkoani Ruvuma Enock Lugenge kushoto akikabidhi jana, madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Titus Ng'oma ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa ajili ya kuwanusuru wanafunzi wa shule za msingi wilayani humo kukaa chini.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Titus Ng'oma kulia akipokea moja kati ya madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa na Benki ya CRDB Tawi la Songea kutoka kwa meneja wa Benki hiyo Enock Lugenge kushoto, ikiwa ni kuitikia wito wa Rais Dkt John Magufuri ya kuwataka wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na serikali yao kupunguza uhaba wa madawati kwa shule za msingi na sekondari hapa nchini,wanaoshuhudia kwa nyuma ni wajumbe wa kamati ya fedha uchumi na mipango wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Titus Ng'oma aliyekaa katikati,meneja wa benki ya CRDB Tawi la Songea Enock Lugenge wa kwanza kushoto,na afisa elimu ya msingi wa wilaya ya Namtumbo Alberto Mbilinyi kulia wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ndogo ya fedha uchumi na mipango ya baraza la madiwani wa halmashauri hiyo mara baada ya benki ya CRDB kukabidhi msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shlingi Mil 5 kwa halmashauri hiyo. Picha na Muhidin Amri
Post a Comment