MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA.
Siku kadhaa zilizopita kiliibuka kisanga kilichopelekea ndoa changa (ya wiki 1) kuvunjika, baada ya kufungua zawadi na kukuta picha mbaya za uchi za 1 kati ya wanandoa hao, akifanya mapenzi na mtu mwingine kabla ya kufunga ndoa. Sisi wote ni mashahidi wa tukio hilo.
Hizo ni baadhi ya athali za kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa.
1. Mimba zisizo rasmi.
2. Utoaji mimba.
3. Kupata magonjwa ya zinaa.
Sio ukimwi tu lakini pia kuna magonjwa mengine ya zinaa mengi tu ambayo ni hatari pia.
4. Ndoa za lazima.
Katika jamii nyingi za kiafrika ata ulaya kijana anapompa binti mimba, wazazi na jamii kwa ujumla inalazimika kumwajibishi kijana huyo kwa kumwambia amchukue binti huyo na kuishi nae milele.
5. Utafiti unaonesha kwamba tendo la ndoa linaadhari kubwa sana kwa vijana wadogo kisaikologia, kijamii na hata kwenye masomo yao. Kwa sababu vijana wadogo hawana uwezo kucontrol hisia na hali ya tendo la ndoa. (Tendo la ndoa huwa-control hao) Ndio maana vijana wakijiushisha katika maswala ya mapenzi nidhamu na tabia zao hugeuka na kualibika (kuwa mbaya) lakini pia kufanya vibaya katika masomo yao.
6. Kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa ni kuvunja maagizo na utaratibu (moja kati ya amri 10) ambazo Mungu aliziweka.
7. Huondoa thamani ya mtu.
Ni fahari ilioje! Pale ambapo unaingua katika ndoa ukiwa bado ni bikra! Hiyo ndiyo zawadi kubwa na yenye dhamani kuliko zote kwa mpenzi wako. Lakini pia hali hiyo inajenga imani kwa mme/mke wako. Tofauti na hapo ni dharau na mashaka.
Upendo wa kweli hungojea. Kama ni kweli anakupenda, bhasi lazima akutakie mambo mema. Awezi kukuhushisha katika mambo ambayo yanaweza kuhatalisha maisha yako ya sasa na ya baabae kama mimba, magonjwa, madhara ya kisaikologia n.k kwa kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Kama kweli anakupenda lazima atangojea mpaka siku ile ya ndoa na kisha mfurahie milele kwa baraka za wazazi, jamii na Mungu mwenyewe.
Post a Comment