Huku Waislamu wanaopoendelea kusherehekea sikukuu ya Eid al-Adha, watu wa Dhaka wanaendelea kupokezana, kupitia kwa mtandao, picha za barabara zilizofurika maji yaliyochanganyana na damu.
Damu inatoka katika wanyama waliochinjwa na kuchanganyika na maji ya mafuriko katika sehemu fulani za mji mkuu wa Banglaeshi.
- Ni kwa nini hili linatendeka?
Zaidi ya mifugo 100,000 walichinjwa katika Dhaka mwaka huu, kulingana na idhaa ya Bengali ya BBC.
Mifugo hawa wengi wamechinjiwa katika barabara au katika maeneo ya kuegeshea magari ya chini katika nyumba za makaazi.
Wakati huohuo kulikuwepo na mvua na upepo wa Monsoon hiyo jana ambao ulisababisha mafuriko jijini.
Mafuriko yamekuwa tatizo kubwa katika sehemu zingine za jiji kwa sababu ya ukosefu wa mitaro ya kutoa maji taka.
Katika mji wa Shantinagar, na maeneo mengine, damu na samadi ya mifugo ilichafua sana barabara ambapo wakaazi wanaonekana wakitembea katika maji yaliyochanganyika na damu yaliyo karibu kuwafikia magotini.
Mafuriko na uchinjaji mifugo ni maswala ya kawaida katika Dhaka, jambo ambalo limewafanya watu wachache tu kuzungumzia uchafu huu wa kupindukia.
- Kwa nini Mifugo wanachinjwa?
Siku kuu ya Eid al-Adha, ni sikukuu ya pili kwa umuhimu kwa Waislamu, ambapo wanasherehekea wakati mtume Ibrahim alionyesha kuwa alikuwa tayari kumtoa kafara mwanawe, Ishmail.
Mbuzi na ng'ombe hununuliwa na familia za Kiislamu kuchinjwa na kumshukuru Allah kwa kumwachilia Ishmail, baada ya imamu kusoma Koran.
Nyama hiyo hugawanywa miongoni mwa familia, marafiki na maskini lakini mabaki mengine na matumbo hutupwa.
- Je hili lishawai kutoka awali?
Karibu kila mwaka kuna kiasi fulani cha damu kwenye barabara za familia zinapochinja mifugo yao.
Uchafu huu hotoweka baada ya siku chache.
Hata hivyo mvua mwaka huu imeongeza uchafu huu na kufanya barabara kuonekana kama zilizojaa damu kila mahali.
Source bbc
Post a Comment