Usiku wa September 24 2016 heshima nyingine ya Tanzania iliandikwa nchini Marekani baada ya aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kushinda tuzo ya kimataifa ya ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award or Sustainable Development‘ ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani.
Kazi ya utoaji wa tuzo hizi ulifanyika katika makao makuu ya umoja wa mataifa New York Marekani ambapo viongozi mbalimbali duniani walishiriki kushuhudia tukio hilo huku Tanzania ikisindikizwa na Waziri wa mambo ya nje Balozi Augustine Mahiga pamoja na mbunge wa viti maalum Anna Lupembe.
Unapoingia na kutoka katika ukumbi ulikuwa unakutana na picha hii
Profesa Tibaijuka na baadhi ya washiriki wakati wa utoaji tuzo
Profesa Tibaijuka akikabidhiwa tuzo hiyo ya heshima
Profesa Tibaijuka akitoa hotuba mbele ya waalikwa
.
Baadhi ya vyombo vya habari Marekani viliripoti tukio hilo kama unavyoweza kujionea hapa kwenye hii video..
Post a Comment