Unknown Unknown Author
Title: Idadi ya wahamiaji waliozama kutoka Misri yaongezeka
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Idadi ya miili ya watu iliopatikana baada ya boti la wahamiaji kuzama kutoka pwani ya Misri Jumatano imefika 162, huku operesheni ya kutaf...
Maafisa wanasema wamewapata watu 163 baada ya boti hilo kuzama kutoka pwani ya Misri
Idadi ya miili ya watu iliopatikana baada ya boti la wahamiaji kuzama kutoka pwani ya Misri Jumatano imefika 162, huku operesheni ya kutafuta miili zaidi ikiendelea.
Boti hilo lilikuwa limewabeba kati ya wahamiaji 450 na 600 lilipozama kilomita 12 kutoka mji wa bandari wa Rosetta.
Lilikuwa linawasafirisha raia wa Misri, Syria, Sudan, Eritrea na hata wahamiaji wa Somalia.
Maafisa wanasema kiasi ya watu 163 wameokolewa lakini walionusurika wameiambia BBC kuwa mamia wengine huenda wamezama.
Boti linalozama katika picha kutoka operesheni ya uokozi ya Umoja wa Ulaya - takriban watu 30 walizamaImage copyrightAFP
Image captionBoti linalozama katika picha kutoka operesheni ya uokozi ya Umoja wa Ulaya - takriban watu 30 walizama
Wanasema wasafirishaji haramu wa binaadamu walimlazimisha yoyote aliyetaka makoti ya kuelea majini kulipa pesa zaidi .
Washukiwa wanne wamekamatwa na polisi kwa kushukiwa kwa mauaji yasio ya makusudi na usafirishaji haramu wa binaadamu, maafisa wa Misri wanasema.
Boti hilo lililo ondolewa kutoka pwani kwa siku tano wakati wahamiaji zaidi walipoletwa, linasemekana kuzama baada ya kundi la mwisho la watu 150 kujazwa ndani.
Mkasa huo unatokea wakati shirika la kulinda mpaka wa Umoja wa Ulaya limeonya kuwa idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaoelekea Ulaya wanatumia Misri kama eneo la kuondoka.
Zaidi ya watu 10,000 wamefariki wakivuka bahari ya Mediterrania kuelekea Ulaya tangu 2014, kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.
bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top