Marekani imesema inasikitika juu ya shambulio lililoongozwa na ndege zake za kivita ambapo, bila kukusudia zililipua kambi za wanajeshi wa Syria.
Wakati huohuo Marekani imekosoa Urusi kwa kuitisha mkutano maalumu wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ikisema hatua hiyo ya Urusi kutaka kuwakosoa Marekani bila sababu maalumu.
Urusi inasema kuwa wanajeshi 60 wa Syria waliuawa katika shambulio hilo la Kaskazini Mashariki mwa Syria.
Makao Makuu ya Kijeshi yanasema kuwa ndege hizo zilidhania kuwa zilikuwa zikishambulia kambi za makundi ya Islamic State, ambazo Marekani ilisema zilikuwa zikitafuta kwa siku kadhaa.
Lakini Urusi inasema kuwa Marekani walikuwa na lengo la kuwasaidia wanachama wa Islamic State na kuongezea kuwa mapatano yake na Marekani kuhusiana na usitishaji wa mapigano umehatarishwa.
Hakuna habari za kuthibitisha idadi ya watu waliouawa.
SOurce bbc
Post a Comment