Mdahalo wa wagombea urais wa Marekani Hillary Clinton wa Democratic na Donald Trump wa Republican ulikuwa kama pambano kati ya wakili na muuza bidhaa, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa Amerika Kaskazini Anthony Zurcher, na wengi wanasema ni kama wakili aliibuka kidedea
Nani bora kati ya wakili na muuza bidhaa
Ni vigumu kukumbuka lakini kabla Bi Clinton ahudumu wadhifa wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, seneta au mama wa taifa , alikuwa ni wakili na wakili mwenye kipaji.
Na kwa miaka hii yote bado anaendesha kampeni yake kama wakili, akiwa anachukua tahadhari na aliye mtulivu, tabia ambayo wakili anahitaji kuwa nayo mahakamani.
Bwana Trump kwa upande mwingine ni muuza bidhaa. Udhaifu uliopo hapa ni kwamba muuza bidhaa huzungumza sana jambo ambalo linaweza kuwa tatizo kwa mda wote wa dakika 90 za mdahalo.
Bi Clinton alionekana kung'aa aliposema kuwa Trump amekataa kuweka wazi kodi zake, akisema kuwa kuna jambo mihimu ambalo Trump hataki nchi ilijue au labda huenda likawa ni jambo baya ambalo anajaribu kulificha.
Kabla ya Trump kuvutwa kwenda kwa suala la kodi, alitumia muda mrefu akijaribu kujieleza na mdahalo ulionekana kumwendea salama.
Hata hivyo Bi Clinton alionekana kung'aa katika sehemu ya kwanza ya mdahalo, alipomhangaisha Trump kuhusu suala la kodi huku vilevile nayo sehemu ya pili ikionekana kuwa changamoto kubwa kwa Republican.
Uhusiano kati ya watu wa rangi tofauti
Suala lilikuwa ni uhusiano kati ya jami za rangi tofauti nchini Marekani, na ndio wakati huu Trump alihitajika kueleza ni kwa sababu gani alikuwa na shaka juu ya uraia wa Rais Obama.
Trump kwa mara nyingine alijaribu kumlamu Bi Clinton kwa kuanzisha uvumi huo mwaka 2008 akisema kuwa anastahili shukran kutoka kwa Obama na wapiga kura weusi wa kwa kuchangia ufumbuzi wa suala hilo.
Bi Clinton alitumia fursa hilo kumshambuli Trump akisema kuwa alionyesha ubaguzi ulio wazi aliposema kuwa rais mweusi wa marekani hakuwa raia wa nchi hiyo.
Nani aliye na tajriba na kuongoza?
Mdahalo ulipoelekea dakika zake za mwisho mwisho suala la ni nani aliye na uwezo wa kuongoza liliibuka. Clinton alijitetea akisema kuwa safari zake nchi za nje na jitihada za kutatua masuala kwa njia ya kidiplomasia vilionyesha kuwa ana uwezo wa kuwa rais.
Alimlaumu Trump kwa kuwaita wanawake nguruwe na mbwa na kwa kudai kuwa wanawake hawastahili mishara sawa ikiwa hawajafanya kazi sawa na wanaume.
Hata hivyo Trump alijibu akisema kuwa matangazo ya Bi Clinton yanampiga vita, lakini badala yake anazidi kufanya vizuri katika kura ya maoni, jambo ambalo halikuridhisha.
Post a Comment