Leo September 15 2016 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV, imemuhoji mtanzania Benjamini Fernandes mwenye miaka 23 anayefanya kazi kwenye taasisi ya Melinda & Bill Gates Foundation inayoendeshwa na tajiri namba moja duniani, Bill Gates ambaye pia ni mwanzilishi wa kampuni ya microsoft na mbunifu mkuu wa programu za kampuni ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani.
Benjamini Fernandes ameeleza namna ambavyo alijituma licha ya kuwa na historia mbaya ya kwenye masomo hapa Tanzania na alipopata nafasi ya kwenda Marekani kusoma alijituma zaidi na akawa anaongoza darasani ambapo baadaye alifanikiwa kuwa mtu wa kwanza barani Afrika kushinda tuzo ya MBA/ World Summit.
>>>Nilisoma Haven peace of academy hapa Kunduchi Dar ess salaam na nilivyokuwa nagraduate nikawa wa mwisho darasani hata wazazi walivyokuwa wakienda shuleni wanaambiwa huyu ni mototo wako mbona anafeli sana mnamfundisha nini nyumbani;-Benjamin Fernandes
>>>Nilipata nafasi moja kwenda nje kusoma waliniambia tunakupa semester moja kwenda collage ukifaulu utaendelea na ukifanya vibaya utarudi…..Bili Gates Foundation walikuja shuleni kutafuta watu wa kufanya kazi naye, mimi nikaenda kuapply. Kulikua na CV za watu 70 zikachukuliwa CV 20 kwaajili ya interview, CV yangu haikuchaguliwa:–Benjamini Fernandes
>>>Mwalimu alinishauri niende pale nikagonge mlango na niongee nao kuwa nataka kuwaona kwa dakika 5 na nilifanya hivyo:-Benjamini Fernandes
Post a Comment