Unknown Unknown Author
Title: Rodrigo Duterte asema "anafurahia kuua" sawa na alivyofanya Hitler
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amelinganisha vita vyake dhidi ya walanguzi wa mihadarati na mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya...
Rodrigo Duterte akiwa Davao
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amelinganisha vita vyake dhidi ya walanguzi wa mihadarati na mauaji ya Wayahudi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Amesema anaweza kuua walanguzi wengi wa dawa hizo za kulevya sawa na alivyofanya Hitler akiua Wayahudi.
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu ... kuna waraibu milioni tatu wa dawa za kulevya. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.
Wayahudi zaidi ya milioni sita waliuawa na Wanazi chini ya Hitler.
Bw Duterte amekuwa akiongoza kampeni kali ya kuua walanguzi na watu wanaotumia dawa za kulevya tangu achukue madaraka mwezi Juni.
Takwimu rasmi zinaonesha watu zaidi ya 3,000 wameuawa kwenye operesheni za polisi au na makundi ya kiraia.
Miili ya waliouawa huachwa hadharani, ikiwa na mabango yaliyoandikwa makosa waliotuhumiwa kutekeleza.
Rais huyo awali amesema anaweza kufurahia sana "kuua wahalifu 100,000" kupunguza viwango vya uhalifu Ufilipino.
'Maneno ya kukera'
Bw Duterte alikuwa akiongea Davao, mji ambao alikuwa meya zamani ambapo alitekeleza sera kali ya kuunga mkono makundi ya kuua wahalifu.
Manila, 21, Agosti 2016Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionWengi wa waliouawa wamekuwa wahalifu au walanguzi wa mihadarati wa ngazi ya chini
Ameambia wanahabari kwamba amekuwa akioneshwa na baadhi ya wakosoaji wake kama "binamu wa Hitler".
"Hitler aliua Wayahudi milioni tatu, kuna waraibu milioni tatu. Ninaweza kufurahia sana kuwaua," amesema.
"Angalau Ujerumani walikuwa na Hitler. Wafilipino hawawezi."
Rodrigo Duterte akibusu bendera Manila (7 Mei 2016)Image copyrightREUTERS
Amesema angependa sana "kumaliza tatizo hilo nchini mwangu na kuokoa vizazi vijavyo".
Matamshi yake yameshutumiwa na makundi ya Wayahudi, shirika la habari la Reuters limeripoti.
bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top