Unknown Unknown Author
Title: Sababu ya wanawake marafiki kupata hedhi pamoja
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Inaaminiwa kwamba wanawake wanaoishi pamoja hatimaye huwa na mizunguko inayofanana ya kila mwezi ya hedhi. Lakini je hili ni kweli ama ni ...
Picha ya mwanamke aliye kwenye hedhi
Inaaminiwa kwamba wanawake wanaoishi pamoja hatimaye huwa na mizunguko inayofanana ya kila mwezi ya hedhi. Lakini je hili ni kweli ama ni jambo linalotokea kwa bahati tu?
Dhana kuhusu mizunguko hiyo ya hedhi ni kwamba vichocheo vya mwili vya mwanamke ama homoni vinavyosababisha hedhi kwa lugha ya kitaalamu-pheromones- hufanya kazi kwa wakati mmoja wanapokuwa na uhusiano wa karibu, na hivyo kuwasababisha kupata hedhi kwa wakati mmoja. Wanawake wengi wamejikuta katika hali hii.
"Nadhani suala hili ni kweli ," anasema Emma. "Tukisema ni suala linalojitokeza kwa bahati basi zitakuwa ni bahati nyingi sana ."
Emma, mwenye umri wa miaka 24, anaishi na wasichana wenzake watano katika chuo kikuu. Anasema kwamba katika kipindi cha miezi michache wote walipata hedhi zao kwa wakati mmoja.
"Ni suala linaloaminiwa na wengi," anasema Alexandra Alvergne, profesa wa masuala ya kibiolojia na maumbile ya binadamu katika chuo kikuu cha Oxford.
chati ya hedhi ya mwanamkeImage copyrightISTOCK
Image captionTafiti nyingine, kuhusu binadamu na watu waliowahi kuishi pamoja zinathibitisha kuwa wanawake wanaoishi pamoja hupata hedhi wakati mmoja
Kuna nadharia mbali mbali kuhusu sababu inayoweza kusababisha wanawake wanaoishi pamoja kupata hedhi wakati mmoja.
Utafiti wa Dkt Martha McClintock mwaka 1971 ulidokeza hili huenda lilikuwa ni kwa sababu wanawake waliokuwa wanaishi pamoja walikuwa na uwezekano kwamba homoni za kila mmoja ziliweza kuathiri za mwenzake miongoni mwa marafiki wa karibu.
Na kwa nini basi hili likawezekana? Nadharia ambayo inakubaliwa na wengi ilikuwa ni uwezo wa ushirikiano uliopo baina ya wanawake katika mambo na kwamba huenda walikata kushirikiana kuzuia kugeuzwa kuwa maharimu na mwanamume mmoja.
Kwa kuoanisha mizunguko yao ya hedhi, hii ina maana kwamba mwanamume mmoja aliye karibu nao hangeweza kuwatungisha mimba kwa pamoja kwani wakati mmoja angelikuwa anamwangazia mmoja na kabla amwangazie yule mwingine, kipindi chake cha kuweza kushika mimba kitakuwa kimepita.
Baadhi ya wasomi hivi karibuni waliamua kuchunguza kwa kina iwapo matokeo ya mzunguko wa hedhi kwa wanawake wanaoishi pamoja yanaweza kuwa ni ya kubahatisha.
Waliangalia taarifa za mizunguko ya hedhi walizokusanya katika kipindi cha miaka sita wakiangazia nyani, ambao wanakaribiana sana na binadamu.
" Walipendekeza nadharia mbili," anasema Alvergne. " Moja ni ya kutumia "msisimuko " ambayo pia ilifahamika kama "mpango wa mabadiliko," ambapo wanawake hubadilisha mzunguko ili kuungana na kushirikiana kama kinga dhidi ya mwanamume mbabe.
"Nadharia nyingine ni ya mtu anayeudhi. Ambapo mienendo yake inaweza kuelezwa kwamba inatokana tu na bahati."
WanawakeImage copyrightISTOCK
Watafiti walilinganisha nadharia hizo mbili kulingana na taarifa zinazochunguzwa.
Walibaini kwamba nadharia kwamba kulingana kwa mzunguko wa hedhi unaweza kuelezwa vyema kwa 'mtu wa kuudhi' ambapo ulinganifu ulitokea kibahati tu ndiyo iliyofaa zaidi.
Utafiti zaidi unaweza kufanyika siku zijazo ambao utafichua zaidi ushahidi kuhusu mizunguko ya hedhi ya wanawake. Lakini kwa sasa watafiti wana shaka kuhusu kuwepo utaratibu au sababu inayosababisha hili.
"Labda kusema ukweli, kile tulichokiona ni jambo la kibahati tu," anasema Alvergne.
Tafiti nyengine, kuhusu binadamu na watu waliowahi kuishi pamoja zilionyesha majibu yanayofanana na hayo.
Lakini kulikuwa na tafiti nyingine ambazo hazikupata ushahidi wa wanawake wanaoishi pamoja na kuwa na urafiki kupata hedhi kwa wakati mmoja.
Source bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top