Unknown Unknown Author
Title: Shambulio la kigaidi latibuliwa Mombasa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wanawake watano waliovalia mabuibui na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika sham...
Shambulio la kigaidi latibuliwa mjini Mombasa
Wanawake watano waliovalia mabuibui na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.
Maafisa wa polisi nchini Mombasa wanasema kuwa walitibua jaribio hilo na kufanikiwa kuwaua wanawake watatu huku wawili wakikamatwa.
Polisi wanasema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kuripoti kuhusu simu ya rununu ilioibiwa.
Na wakati malalamishi yao yalipokuwa yakichukuliwa mmoja wao alichukua kisu na kuwadungu maafisa wawili wa polisi ,huku mwengine akiwarushia polisi waliokuwa wakichukua malamishi hayo bomu la petroli.
Polisi wanasema kuwa waliwafyatulia risasi na kuwaua wote.
Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.
Kumekuwa na mashambulio kadhaa katika eneo la pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni mengi yakifanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab.
Source bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top