Unknown Unknown Author
Title: SOMALIA YARUHUSU MIRUNGI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Serikali ya Somalia imeondoa marufuku iliyokuwa imewekwa dhidi ya mirungi kutoka nchi jirani ya Kenya. Mirungu ambayo pia hufahamika kam...
Miraa
Serikali ya Somalia imeondoa marufuku iliyokuwa imewekwa dhidi ya mirungi kutoka nchi jirani ya Kenya.
Mirungu ambayo pia hufahamika kama miraa, hutumiwa sana Somalia lakini huwa haikuzwi huko.
Uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo iliyowekwa wiki iliyopita ulitangazwa baada ya marais wa nchi hizo mbili, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Hassan Sheikh Mohamoud, pambizoni mwa mkutano wa IGAD.
Mkutano huo wa muungano wa mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na pembe ya Afrika ulikuwa wa kwanza kuandaliwa mjini Mogadishu tangu kuanzishwa kwa muungano huo.
Usafirishaji wa mirungi hadi Mogadishu, biashara ya thamani ya karibu dola nusu milioni kila siku, inatarajiwa kurejelewa Jumatano.
Marufuku iliyokuwa imewekwa iliwaumiza sana raia wanaoitumia pamoja na wafanyabiashara nchini Somalia sawa na wakuzaji nchini Kenya.
Bei ya mirungi ilikuwa imepanda pakubwa.
Ndege 15 za kusafirisha miraa huingia Mogadishu kila siku zikiwa zimebeba magunia 12,000 ya miraa ya thamani ya $400,000 (£298,000) kwa mujibu wa mtetezi wa haki za wauzaji miraa Somalia Abukar Awale.
Source bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top