Unknown Unknown Author
Title: WAFUNGWA WALIPWA NCHINI AUSTRALIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wafungwa katika jela moja nchini Australia wamegoma wakidai malipo. Wafungwa wote katika jela ya Barwon mjini Victoria wanahitajika kufa...
Jela ya Barwon nchini Australia
Wafungwa katika jela moja nchini Australia wamegoma wakidai malipo.
Wafungwa wote katika jela ya Barwon mjini Victoria wanahitajika kufanya kazi isipokuwa wanapokuwa wagonjwa sana ama wakati wanapokuwa wazee sana .
Wafungwa waliogoma wanasema kuwa dola 6.90 walizoahidiwa katika makubaliano mapya hazitoshi kusimamia gharama yao ya maisha.
Upinzani nchini humo unataka walazimishwe kurudi kufanya kazi ,ukisema kuwa wananchi wamekasirishwa na hatua kwamba wafungwa hao wana uwezo wa kugoma.
Malipo ya dola 9 kwa siku ambayo wafungwa hao wameahidiwa ,kulingana na kazi zao na saa wanazofanya kazi ,ni ongezeko la malipo ya sasa ya kati ya dola 6.50 na dola 8.95,lakini imekosolewa kutotosha na wafungwa na wafuasi wao.
Malipo hayo ni ya kiwango cha chini sana ikilinganishwa na majimbo mengine nchini Australia na hayafikii gharama zao zinazoongezeka kila uchao,alisema Brett Collins,msemaji wa kundi linalopigania haki za wafungwa.
Source bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top