Unknown Unknown Author
Title: Mchina afariki baada ya kukandamizwa na mtambo wa kushindilia lami Arusha
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ujenzi wa barabara ya kuanzia Tengeru Arusha hadi Taveta Voi ya ukubwa wa km 234.3 iliyozinduliwa March 3 mwaka huu na Rais John Magufuli,...

Ujenzi wa barabara ya kuanzia Tengeru Arusha hadi Taveta Voi ya ukubwa wa km 234.3 iliyozinduliwa March 3 mwaka huu na Rais John Magufuli, wakati ujenzi ukiendelea kumetokea ajali ambapo Raia wa china Eng. Pil soo shin amekandamizwa na mtambo wa kushindilia lami na kufariki dunia. 
Kwa mujibu wa balozi wa eneo la kwa mrefu ambaye pia ni shuhuda amesema marehemu alikuwa akisimamia zoezi la kushindilia lami kwenye barabara na mwendesha mtambo hakumuona, jambo lililopelekea  suruali yake kushikwa na nondo iliyokuwa karibu hivyo akaangukia barabarani na mtambo ukamkanyaga.
Jeshi la polisi kupitia kwa kaimu kamanda wa polisi Arusha Yusuph Ilembo amesema kwamba mtuhumiwa aliyesababisha kifo hicho kwa uzembe bado anashikiliwa na polisi na uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani.
1111
1111

mashuhuda wa tukio 
222
333

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top