Unknown Unknown Author
Title: Rais Obama aumbuliwa na mwanae
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Marekani Barack Obama amesema bintiye wa miaka 15, Sasha, alimcheka kwenye ujumbe aliowatumia marafiki zake kupitia mtandao wa kij...
Sasha Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amesema bintiye wa miaka 15, Sasha, alimcheka kwenye ujumbe aliowatumia marafiki zake kupitia mtandao wa kijamii wa Snapchat.
Kiongozi huyo wa Marekani amesema Sasha alimpiga video akijadili mtandao huo wa kijamii kwenye dhifa ya familia na kisha, kisiri akawatumia marafiki zake akiwa ametoa maoni yake.
Hii si mara ya kwanza kwa rais huyo kujadili shughuli za mtandaoni za bintiye huyo.
Mwezi Julai, alisema kwamba Sasha hutumia Twitter na kusababisha baadhi ya vyombo vya habari kujaribu kutambua akaunti ya Sasha kwenye Twitter.
Hadi wa leo imesalia kuwa siri.
Maneno hasa aliyoandika Sasha kwenye Snapchat hayajafanywa wazi.
Ujumbe unaopakiwa kwenye mtandao huo wa kijamii huwa unatoweka baada ya kutazamwa na anayelengwa au baada ya kipindi kifupi, lakini kuna njia za kukwepa hilo.

Picha ya upweke

Rais Obama alisimulia kuhusu kisa hicho cha Snapchat kwenye mahojiano katika kipindi cha runinga cha Jimmy Kimmel Jumatatu.
President ObamaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionRais Obama akihojiwa na Jimmy Kimmel
"Sasha alinipa maagizo Snapchat," alisema.
"Jioni moja wakati wa dhifa ya jioni ya familia tumeketi hapo, na nilikuwa nimesoka kuhusu jinsi Snapchat imekuwa maarufu kwa watu wa rika lake. Kwa hivyo nikamwambia: 'Sasa, niambie kuhusu Snapchat.'
"Hivyo, anaanza kunifafanulia - unaweza kubadilisha sura yako, na hili na lile.
"Na mwishowe, Michelle na mimi tumeketi hapo. Na nikasema: 'Si inafurahisha sana?'
"Na nikaanza kumwambia Michelle kuhusu athari za mitandao ya kijamii.
"[Na] kisha nikagundua kwamba alikuwa anatunakili kwenye video wakati wote, na kisha akawatumia marafiki zake baadaye: 'Huyu ni babangu akitufundisha kuhusu mitandao ya kijamii.'
"Na akajipiga picha yake mwenye akionekana mwenye upweke."
Rais aliongeza kwamba mkewe alijiunga na Snapchat mwezi Juni, na bintiye mkubwa alikuwa "amependa" ujumbe huo.
Michelle Obama
Image captionUjumbe kwenye Snapchat huonekana kwa muda tu
Jimmy Kimmel, alifanya mzaha kwamba kisa hicho kilikuwa sawa na ukiukaji wa masharti ya kiusalama.

Kufichuliwa kwa barua pepe

Rais pia alisema simu yake ya iPhone amekuwa tu akiitumia kupokea barua pepe na kuchakura mtandaoni na kwamba hawezi kupiga picha, kucheza muziki au kupiga simu.
"Kanuni yangu kipindi changu cha uongozi imekuwa, nachukulia kuwa siku moja, wakati mmoja, kuna mtu atasoma barua pepe hii," amesema.
"Hivyo, huwa situmi barua pepe yoyote ambayo siwezi nikafurahia ikigonga vichwa vya magazeti."
President ObamaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionHuduma nyingi kwenye iPhone ya rais zimefungwa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top