Unknown Unknown Author
Title: Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu ajibu kauli ya Rais Magufuli
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mara nyingine tena Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu amegongana tena angani na rais Magufuli. Wakati rais Magufuli akiwa...

Kwa mara nyingine tena Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu amegongana tena angani na rais Magufuli.

Wakati rais Magufuli akiwa amepiga marufuku Mashirika ya Umma kuwa na akaunti maalum kwenye mabenki ya biashara, Gavana huyo wa BoT amesema hakuna kosa lolote kuwa na akaunti hizo zijulikanazo kama "fixed deposit" huku akisisitiza kuwa ni vigumu faida itokanayo na fedha hizo kuingia mifukoni mwa wachache.

Gavana huyo wa BoT ni miongoni mwa wajumbe wa iliyokuwa bodi ya wakurugenzi wa TRA ambao walifungua akaunti maalum kwa ajili ya fedha za miradi ya TRA kwenye mabenki ya biashara zaidi ya Tshs. Bilioni 8. 5 ambapo kitendo hicho kilimkasirisha rais Magufuli na kuamua kuivunja bodi hiyo.

Kitendo cha rais Magufuli kuzuia mashirika ya umma kuwa na akaunti maalum kwenye mabenki ya biashara kimetajwa kuwa na madhara makubwa ambapo ndicho hasa kilichoathiri mzunguko wa fedha na kuporomoka kwa uchumi.
Jmiiforum

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top