Unknown Unknown Author
Title: MIKOA INAYOONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mikoa ya  Tabora, Katavi na Rukwa  imetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hiyo ni kwa muji...

Mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.

Taarifa hiyo ilitolewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes Wilbroad katika mafunzo ya siku moja ya viongozi wa dini yaliyofanyika Nzega.

Alisema mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni Rukwa wenyeasilimia 6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia 5.2 na Tabora asilimia 5.1.

Alitaja sababu zinazochangia maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi na kukithiri  imani potofu za ushirikina.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top