Unknown Unknown Author
Title: Ugomvi mkubwa watokea kanisani Arusha baada ya Bwana Harusi akidaiwa kufunga ndoa ya pili
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Weekend hii siku ya Jumamosi mkoani Arusha wakati ndoa ikifungwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri ‘KKKT’, Usharika wa Usa River, wil...

Weekend hii siku ya Jumamosi mkoani Arusha wakati ndoa ikifungwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri ‘KKKT’, Usharika wa Usa River, wilayani Arumeru ziliibuka vurugu baada ya pande mbili zilizokuwa zikivutana upande mmoja ukidai bwana harusi anafunga ndoa ya pili na Bibi harusi aitwaye Agnes Kaaya.
Ndoa hiyo iliyokuwa ikifungwa majira ya mchana iliingia dosari  baada  mwanamke aliyejulikana kwa jina la Aneth Kimaro akiwa na kundi na watu mbalimbali wakiwemo watoto wake kudai kuwa Bwana Harusi ni mume wake wa ndoa.
Vurugu iliendelea kwa saa mbili zaidi kuanzia saa nane hadi za kumi jioni huku waumini wa pande zote mbili wakirushiana maneno makali mpaka polisi wa kutuliza ghasia kituo cha usa river kuingilia kati na kuwakamata kundi lililovamia kanisani hapo akiwemo mke wa zamani, Aneth Kimaro ambao kwa pamoja wanashikiliwa na polisi wa kituo cha polisi Usa river.
Akizungumzia tukio hilo Bwana harusi, Ngarame Meena alikiri kumtambua Aneth Kimaro kama mke wake wa ndoa lakini alisema waliaachana kutokana na ndoa yao kutawaliwa na migogoro mikubwa na yeye kuamua kukimbilia mahakamani kuiomba mahakama ivunje ndoa hiyo ambayo ilifungwa mwaka 1993.
AAidha ameongeza kuwa ndoa yake ilikumbwa na migogoro mingi tangu mwaka 1996 na ameshasuluhisha maeneo mbalimbali ikiwemo kwa mkuu wa wilaya ya Arusha, Meru na baraza la kata la ndoa bila mafanikio baadaye aliamua kwenda mahakamani kuomba ndoa hiyo ivujwe na ilipofika November 27  2015 mahakama ilitoa hati ya kuvunja ndoa hiyo na yeye kuwa huru kufunga ndoa nyingine.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top