Unknown Unknown Author
Title: Waziri mkuu ajiuzulu
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serika...
Wadhifa wa bwana Ponyo utachukuliwa na mwanachama wa upinzani
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama vya upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.
bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top