Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaunga mkono pendekezo la kupunguza sauti za wito wa ibada 'adhan', akisema kuwa amepokea malalamishi ya kelele.
Baadaye siku ya jumapili kamati ya serikali itajadili mswada ulio na mpango huo.
Vyombo vya habari vya Israel vinasema kuwa mikakati hiyo itazuia misikiti kutotumia vipaza sauti mara tano kwa siku ili kuwaita wafuasi wa dini hiyo kufanya ibada.
Wakosoaji wanasema hatua hiyo itakuwa ya ukadamizaji.
Sheria hiyo itaathiri dini zote lakini itatumika sana miongoni mwa wito wa ibada miongoni mwa waislamu au 'adhan'.
Adhan ya kwanza hufanyika mapema alfajiri huku ya mwisho ikifanyika baada ya jua kutua.
Takriban asilimia 17.5 ya raia wanaoishi Israel ni Waarabu na wengi wao ni Waislamu.
bbc
Post a Comment