Unknown Unknown Author
Title: ZIJUE DALILI KUU 7 ZA MTU AMBAYE ATACHELEWA SANA KUFANIKIWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
1. Siku zote ana pesa za  kununua vocha  na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakini  hana PESA  za kununua kitabu kitakachomuonge...

1. Siku zote ana pesa za kununua vocha na kuweka vifurushi,ana pesa za kununua nguo  lakini hana PESA za kununua kitabu kitakachomuongezea maarifa.

2. Siku Zote ana muda wa kuchart watsapp, kuangalia Movie, kusoma magazeti na Kupiga stori za mpira ama za wasanii lakini hana MUDA wa Kusoma kuhusu taalumayake ama mambo ya kumuongezea ujuzi.

3. Siku zote akiona waliofanikiwa anawatuhumu aidha wameiba, ni freemason ama wana bahati katika maisha. Huwachukia na hataki kujifunza Kwao.

4. Siku zote hupenda kuhalalisha kufeli kwake kwa kujitetea, kulaumu uchumi, wazazi, serikali au amerogwa.

5. Siku Zote Hujiona anajua Kuliko Mtu Yeyote Yule na hapendi Kujifunza kwa wengine. Huongea sana Kuliko Kusikiliza.

6. Kila anachoingiza anatumia, ukimwambia kusave ama kuwekeza anasema ngoja nipate cha ziada nitaanza kesho.

7. Anajua mambo mengi sana, anajua stori za mafanikio, anasoma vitabu lakini hafanyii kazi ama anafanyia kazi kidogo sana katika kile anachokijua.

Je Unayo dalili mojawapo kati ya hizo?
Amua kubadilika ishi au fanya ukijua kesho ipo ....

NDOTO YAKO INAWEZEKANA, CHUKUA HATUA.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top