Unknown Unknown Author
Title: Alichokizungumza Waziri wa Mambo ya Ndani Congo kuhusu madereva waliotekwa
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jana ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September ...

Jana ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September 16 habari zilizoripotiwa na BBC Swahili zimedai kuwa watu wameokolewa na jeshi la nchi hiyo. 
BBC imezungumza na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambapo kuwa madereva wote wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wako salama. BBC imesema utekaji wa madereva hao ulifanywa na watu wenye silaha katika kijiji cha Matete kuelekea Namoya kilichopo Mji wa Kivu Kusini Mkoa wa Manyema.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo alipoongea na BBC kwa njia ya Simu, amesema ni magari saba ya kampuni ya Simba inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji kutoka Tanzania ndio yaliyochomwa. 
Waziri huyo amesema tukio hilo halijafanywa na waasi kama ilivyoanza kuripotiwa, ila ni majambazi tu ndio waliofanya tukio hilo.
>>>Ni majambazi tu wanatoka porini walipoona magari yanatembea wakayasimamisha katikati ya pori na kuangalia kama kuna pesa wanyang’anye lakini hawakukuta pesa wakaamua kuwachukua madereva na kukimbia nao porini kisha wakayachoma magari 6 na moja halikuteketea.:- Waziri Mambo ya Ndani Congo
Source millardayo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top