Maduka ya chakula yanayouza 'Hot Dog' nchini Malaysia yametakiwa kubadili jina la chakula hicho la sivyo kiorodheshwa miongoni mwa vyakula haramu.
Idara ya maendeleo ya kiislamu nchini humo,imesema kuwa inatekeleza uamuzi huo baada ya malalamishi kutoka kwa Waislamu wanaotalii.
Mkurugenzi Sirajuddin Suhamme alisema kuwa jina hilo linaweza kuzua utata.
''Katika Uislamu,mbwa ni mnyama mchafu kwa hivyo jina hilo haliweza kuhusishwa na chakula halali'',alisema.
Maelezo ya chakula kilicho halali nchini Malaysia yanasema: Chakula kilicho halali hakiwezi kupewa jina linalohusishwa na vyakula haramu kama vile nyama ya nguruwe,pombe na vyakula vingine vinavyoweza kuzua utata,vilisema vyombo vya habari.
Waislamu walio wengi hufuata Uislamu wa wastani lakini tabia za kihafidhina zinaongezeka miongoni mwao.
Post a Comment