Unknown Unknown Author
Title: Wasiwasi kuhusu chombo cha Ulaya kilichoenda Mars
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wasiwasi umezidi kuhusu hatiamya chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikuwa safarini kwenda sayari ya Mars, na ambacho k...
Mchoro
Wasiwasi umezidi kuhusu hatiamya chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikuwa safarini kwenda sayari ya Mars, na ambacho kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo Jumatano.
Hii ni baada ya mawasiliano na chombo hicho kukatika.
Wataalamu wanasema mawasiliano na roboti iliyo kwenye chombo hicho cha Schiaparelli yalikatika chini ya dakika moja kabla ya wakati ambao chombo hicho kilitarajiwa kutua katika sayari hiyo.
Setilaiti zinazoizunguka sayari ya Mars zimejaribu kufanya uchunguzi kubaini hatima ya chombo hicho kilichojaribu kutua, bila mafanikio.
Chombo hicho kilikuwa na muda wa chini ya dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita 21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua salama kwenye sayari hiyo.
Moja ya setilaiti za Marekani zilijaribu kuwasiliana na Schiaparelli lakini hakuna majibu yaliyopatikana.
Kuna wasiwasi kwamba roboti hiyo ilianguka vibaya kwenye sayari hiyo na kuharibika.
Shirika la Anga za Juu la Ulaya hata hivyo bado linasema ni mapema sana na linaendelea kuwa na matumaini.
Wahandisi na wataalamu wengine watajaribu kufanya uchunguzi, sana kwenye mifumo yao ya kompyuta, kubaini ni kwa nini mawasiliano yalikatika na kisha wajaribu kuyarejesha.
Shughuli hii yote inaweza kuchukua siku kadha.
Sehemu ya ndaniImage copyrightESA
Baadhi ya maelezo muhimu yatatoka kwa chombo mama kilichokuwa kimebeba chombo cha Schiaparelli, ambacho kwa Kiingereza kinaitwa Trace Gas Orbiter (TGO).
Chombo cha Schiaparelli kilichokuwa kinaenda kutua, chombo cha TGO kilikuwa kinajiweka sawa katika anga ya Mars. Lakini bado kulikuwa na mawasiliano kati yake na Schiaparelli.
Mawasiliano hayo yanaweza kutoa maelezo muhimu kuhusu yaliyojiri chombo hicho kilipojaribu kutua.
Wataalamu wa ESA wakishirikiana na wale waliounda Schiaparelli walitathmini data usiku kucha.
ArtworkImage copyrightESA
Image captionMchoro wa roboti ya Schiaparelli
Mkuu wa wataalamu waliosimamia mradi huo Paolo Ferri aliambia wanahabari Darmstadt, Ujerumani kwamba: "Watu watakesha wakitathmini data. Nina imani maelezo haya yatatueleza ni nini kilikwama wakati wa kutua na kukatiza mawasiliano. Tutafahamu vyema kesho iwapo chombo hicho kimetoweka kabisa au kama kuna juhudi tunaweza kufanya kufufua mawasiliano."
Jaribio la awali la ESA kupeleka chombo katika sayari hiyo lilifanyika mwaka 2003, kwa kutumia chombo cha Uingereza cha Beagle-2.
Chombo hicho kilifanikiwa kutua salama lakini kikashindwa kufungua mitambo yake ya kawi ya jua vyema na hivyo mawasiliano yakakatika.

Kuchunguza dalili za uhai

Chombo Schiaparelli, ambacho kilipaa kutoka duniani mwezi Machi, kilitarajiwa kufanya uchunguzi kubaini iwapo gesi ya Methane ambayo imepatikana katika anga ya sayari hiyo inatokana na shughuli ya kijiolojia au inatokana na viumbe hai.
Mambo yote yakienda ilivyopangwa, wataalamu wanapanga baadaye kurusha mtambo wa kusafiri juu ya sayari, kwa kimombo rover, ambao utatumiwa kuchimba chini ya ardhi ya Mars.
Mtambo huo, utaunganishiwa nchini Uingereza, unaweza kurushwa mwaka 2018 au ukichelewa mwaka 2020.
Uchunguzi wa awali wa setilaiti zinazozunguka dunia na rover ya Curiosity ya Marekani umebaini kuwepo kwa haidrokaboni ingawa za vipimo vya chini sana katika sayari hiyo.
Moja ya mambo yanayoweza kuwa yanachangia kuwepo kwa gesi hizo ni shughuli za kijiolojia ndani ya sayari hiyo ambapo maji yanaweza kuwa yanachanganyikana na mawe na kuzalisha gesi ya haidrojeni ambayo baadaye inageuka na kuwa methane.
Jambo jingine linaloweza kuwa linasababisha kuwepo kwa gesi hiyo ni kuwepo kwa viumbe hai.
Sehemu kubwa ya gesi ya methane duniani hutokana na viumbe hai.
bbc

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top